OCHA yahofia athari za kurusha mabomu kwenye mji wa Aleppo, Syria

30 Julai 2012

Mratibu Mkuu wa Misaada ya Kibindam katika Umoja wa Mataifa, Valerie Amos, ameelezea kusikitishwa kwake na mashambulizi ya mizinga na silaha zingine nzito nzito kwa mji wa Aleppo, ambao ndio mji wenye idadi kubwa zaidi ya watu nchini Syria, pamoja na mji mkuu Damascus na miji mingine jirani. Katika taarifa yake, Bi Amos amesema watu wengi sasa wametafuta makazi ya muda katika mashule na majengo mengine ya umma yaliyopo kwenye maeneo salama.

Amesema watu hawa wanahitaji chakula kwa dharura, pamoja na malazi, maji ya kunywa na vifaa vya usafi. Ametoa wito kwa pande zote husika katika mapigano kuhakikisha kuwa hazilengi raia, na kwamba kuna usalama kwa mashirika ya kibinadam kuweza kuwafikishia waathirika wa mapigano misaada ya dharura.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud