Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wasomi wana Wajibu wa kufanya kwenye Vita dhidi ya njaa:FAO

Wasomi wana Wajibu wa kufanya kwenye Vita dhidi ya njaa:FAO

Mkurugenzi mkuu wa shirika la kilimo na mazao la Umoja wa Mataifa FAO, Jose Graziano da Silva amewataka wasomi kujihusisha kwenye utafiti kuhusu umaskini sehemu za vijijini na pia kuhusu masuala ya wakulima wadogo kwenye chakula na biashara ya kilimo. Da Silva anasema kuwa moja ya changamoto zilizo kwa sasa ni kutumiwa kwa elimu ya kusoma katika kuboresha maisha ya watu sehemu za vijijini kote duniani. Ameongeza kuwa kuwashirikisha wakulima wadogo kwenye mifumo ya kilimo na chakula pia ni suala ambalo linawahitaji wasomi. Jason Nyakundi na taarifa kamili.

(SAUTI YA JASON NYAKUNDI)