Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanaohusika kwenye ghasia nchini Syria watachukuliwa hatua za kisheria:Pillay

Wanaohusika kwenye ghasia nchini Syria watachukuliwa hatua za kisheria:Pillay

Kamishina mkuu wa haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa Navi Pillay ameelezea wasi wasi wake kutokana na hatari inayowakodolea macho raia nchini Syria wakati ghasia zinapoendelea kusambaa kwenye miji mingi na vijiji ikiwemo miji mikubwa zaidi nchini humo ya Damascus na Aleppo.

Pillay ameitaka serikali ya Syria na upinzani kulinda maisha ya raia na kuheshimu sheria ya kimataifa la sivyo wawajibike. Amesema kuwa serikali ina wajibu wa kulinda raia kutokana na kila aina ya ghasia na kuongeza kuwa raia na mali yao ikiwemo nyumba, biashara , shule na sehemu za kuabudu vinastahili kulindwa kutoka na kila aina ya ghasia. Rupert Colville ni msemaji wa Afisi ya Kamishna Pillay

(SAUTI YA  RUPERT COLVILLE)