Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban Aomboleza Kifo cha Rais wa Ghana

Ban Aomboleza Kifo cha Rais wa Ghana

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon leo amesema kuwa amehuzunika na kusononeshwa na taarifa za kufariki dunia kwa rais wa Ghana John Atta Mills na ametuma salamu za rambi rambi kwa wananchi wa taifa hilo.

Amesema jamii itaendelea kumkumbuka daima kiongozo huyo ambaye alijitolea muda wote kuwatumikia watu wa taifa lake.

Amesema katika kipindi hiki kigumu Umoja wa Mataifa uko nyuma ya wananchi wa taifa hilo na utaendelea kuunga mkono michango yote ya magauezi ya kiuchumi na kisiasa yanayotekelezwa sasa.

Kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari, kiongozi huyo aliyekuwa na umri wa miaka 68 alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kansa ya koo.Alikutwa na umauti wakati akiwa katika hispitali moja mjini Accra. Alitwaa madaraka kwa mara ya kwanza mwaka 2009.