Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uhalifu wa Kimataifa ni Biashara yenye thamani ya dola bilioni 870 kila mwaka:UNODC

Uhalifu wa Kimataifa ni Biashara yenye thamani ya dola bilioni 870 kila mwaka:UNODC

 Afisi ya Umoja wa Mataifa kuhusu madawa na uhalifu, imezindua leo kampeni ya kimataifa ya kuwahamasisha watu, ambayo inaangazia hasa zaidi kiwango na gharama ya uhalifu wa kimataifa wa kupangwa. Kampeni hiyo ambayo inatoa maelezo zaidi kuhusu uhalifu wa kimataifa, ambao unatajwa kama tishio kwa amani, usalama wa kibinadamu na maendeleo, na ambao umefanywa kuwa biashara ya mabilioni ya fedha.

Inaonyesha hasa gharama ya tatizo hili la kimataifa kifedha na kwa kijamii, kupitia matangazo ya video na taarifa zinazowalenga waandishi wa habari. Kampeni hiyo inasema mitandao ya uhalifu wa kupangwa, ambao unakadiriwa kuwa na thamani ya dola bilioni 870 kila mwaka, inafaidika kutokana na uuzaji wa bidhaa haramu pale zinapohitajika bidhaa hizo. Fedha hizo ni mara sita zaidi ya fedha rasmi zinazotolewa kama misaada ya kufadhili maendeleo. Monica Morara na taarifa kamili.

(SAUTI YA MONICA MORARA)