Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wengi Wanahatarisha Maisha wakijaribu Kukatiza Pwani ya Caribbean

Wengi Wanahatarisha Maisha wakijaribu Kukatiza Pwani ya Caribbean

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na wakimbizi UNHCR limeelezea wasiwasi wake kutokana na matukio ya kupoteza maisha inayowaandama wale wanaochukua jaribio la kukatiza katika pwani ya Caribbean wakikimbia hali ngumu nchini Haiti.

Ripoti za hivi karibuni zinaonyesha kuwa mwamake mmoja alifariki dunia pale boti alilokuwa akisafiria lilipozama maji . Boti hilo lilikuwa limechukua watu 100 raia wa Haiti, lilikumbwa na mkasa huo karibu na Bahamas.

Ama kiasi kingine cha watu zaidi ya 12 wamearifiwa kupoteza maisha katika eneo la Bahamian na maji ya Marekani wakati wakiwa safarini kukaribia fukwe ya Florida.

Mamia ya watu wanalazimika kukimbilia nchi za mbali wakikimbia hali ngumu ya maisha iliyosababishwa na tetemeko kubwa la ardhi liliipiga Haiti miaka miwili iliyopita.