Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ubaguzi kwenye mashindano watajwa kuwa wa kushangaza

Ubaguzi kwenye mashindano watajwa kuwa wa kushangaza

Mtaalamu wa Umoja wa Mataifa kuhusu ubaguzi Mutuma Ruteere amesema kuwa ubaguzi kwenye mashindano ni tatizo kubwa na huenda ukaathiri mashindano ya olimpiki yanayokuja iwapo hatua za dharura hazitachukuliwa.

Kupitia kwa ripoti kwa baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa bwana Ruteere alitaja baadhi ya matukio yaliyoshuhudiwa wakati wa mashindano ya kombe la Ulaya nchini Ukrain na Poland akiongeza kuwa mengi yanahitaji kutekelezwa ili kumaliza ubaguzi wakati wa mashindano.

Joshua Mmali wa idhaa hii alipata fursa ya kuzungumza na Bwana Rutere na kumuuliza kuhusu mapendekzo aliyotoa kwa Baraza la Haki za binadamu ili kupambana na tatizo la ubaguzi: