Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WFP na Washirika Waendelea na Usambazaji wa Chakula eneo la Sahel

WFP na Washirika Waendelea na Usambazaji wa Chakula eneo la Sahel

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP na washirika wengine wanatekeleza mpango wa kuwafikia zaidi ya watu milioni 10 na misaada ya chakula nchini Mali na eneo la Sahel magharibi wa Afrika. WFP ina mpango wa kuwasaidia watu milioni 1.3 wakiwemo wakimbizi wa ndani 300,000 hadi mwishoni mwa mwaka huu.

Usambazaji wa chakula unaendelea kwenye sehemu za Mopti, Koulikaro na Kayes na utaanza hivi karibuni kwenye sehemu za Segou na Sikasso. Pia mwezi Juni WFP ilianzisha usambazaji wa chakula kwa lengo la kuboresha lishe kwa watu walioathirika na njaa. George Njogopa na taarifa kamili.

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)