Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wataalamu wa UM wataka Hatua Kuendeleza Haki za Wanawake katika Serikali za Mpito

Wataalamu wa UM wataka Hatua Kuendeleza Haki za Wanawake katika Serikali za Mpito

Kundi la wataalamu wa Umoja wa Mataifa linalohusika na ubaguzi wa wanawake kisheria na katika vitendo, limesema kuwa vipindi vya mpito kisiasa hutoa fursa ya kipekee ya kuendeleza haki za binadamu za wanawake, licha ya kuwepo hatari kurudi nyuma na aina mpya za ubaguzi.

Wakitoa ripoti yao ya kwanza ya kila mwaka kwa Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa, Msimamizi wa kundi hilo la wataalam kuhusu ubaguzi wa wanawake katika sheria na vitendo, Kamala Chandrakirana, amesema desturi nzuri ni pale mataifa yanapochukua fursa zilizopo na kuendeleza haki za binadamu za wanawake, na kuepukana na kurudi nyuma kwa njia yoyote ile. George Njogopa anaripoti

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)