Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Pillay aitaka Serikali ya Sudan Kuheshimu Haki za Binadamu

Pillay aitaka Serikali ya Sudan Kuheshimu Haki za Binadamu

Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu, Navi Pillay, ametoa wito kwa serikali ya Sudan kuhakikisha kuwa maandamano yaliyopangwa kufanyika siku ya Ijumaa yanaruhusiwa kufanyika kwa njia ya amani, bila vikosi vya usalama kutumia nguvu na kuwakamata watu kwa halaiki kama ilivyokuwa wiki mbili zilizopita.

Bi Pillay amesema watu wengi, wakiwemo wanaharakati wa haki za binadamu, waandishi habari, wanafunzi na wanasiasa wa upinzani wamekuwa wakikamatwa tangu maandamano yalipoanza mjini Khartoum Juni 17. Jason Nyakundi anaripoti

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)