Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Waathirika kwa Machafuko Kaskazini mwa Mali Wakumbukwa

Waathirika kwa Machafuko Kaskazini mwa Mali Wakumbukwa

Kiasi cha dola za kimarekani 770,000 na kingine 70,000 kinatazamiwa kutolewa kwa ajili ya kulipiga jeki shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na wakimbizi UNHCR ambalo linatazamia kutoa misaada ya dharura kwa zaidi ya familia 25,000 zilizokosa makazi nchini Mali kutokana na machafuko yaliyozuka katika eneo la kaskazini mwa nchi hiyo.

Kiasi hicho cha fedha kimetolewa kwa ushirikiano wa pamoja baina shirika la misaada la Marekani USAID na mfuko wa kudhibiti majanga ya dharura wa Umoja wa Mataifa.

Maeneo yanayotazamiwa kupewa kipaumbele ni pamoja na maeneo ya chakula, madawa, usafiri na huduma nyingine za kijamii ikiwemo pia kuendelea kuwatafuta wale waliopotea.

Zoezi hili linatazamiwa kufanywa kwa ushirikiano baina ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR na wahisani wengine wa misaada ya usamaria mwema.