Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Idadi ya waliokufa Kutokana na Ugonjwa wa H1N1 bado haijulikani:WHO

Idadi ya waliokufa Kutokana na Ugonjwa wa H1N1 bado haijulikani:WHO

Shirika la afya duniani WHO linasema kuwa bado haijabainika ni watu wangapi walioaga dunia kutokana na ugonjwa wa homa ya nguruwe wa H1N1 kati ya mwaka 2009 na 2010. Hii hi kutokana na sababu kwamba ugonjwa wa H1N1 hauorodheshi kama unaosababisha vifo kama maradhi mengine. Hata hivyo kulingana na utafiti wa makala ya Lancet ni kuwa idadi kamili ya waliokufa kutokana na ugonjwa wa H1N1 tangu mwaka 2009 ni mara kumi na tano zaidi. Utafiti huo unakadiri kuwa watu 284,400 walikufa mwaka ambao virusi hivyo vilianza kusambaa duniani. Fadella Chaib ni msemaji wa WHO akiwa mjini Geneva

(CLIP ya CHAIB FADELLA)