Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

FAO yachukua hatua za Kuzuia Kusambaa kwa Ugonjwa wa Mbuzi na Kondoo

FAO yachukua hatua za Kuzuia Kusambaa kwa Ugonjwa wa Mbuzi na Kondoo

Shirika la kilimo na mazao la Umoja wa Mataifa FAO linajiandaa kutoa huduma za dharura kwenye Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo kukabiliana na kuenea kwa ugonjwa ujulikanao kama Peste des Petits ruminants ugonjwa unaoathiri mbuzi na kondoo.

Ugonjwa huo unatajwa kuhatarisha usalama wa chakula nchini DRC na huenda ukasaamba kwenda mataifa ya kusini mwa Afrika ambapo ugonjwa haujawai ripotiwa. Kulingana na idara ya serikali inayohusika na afya ya wanyama ugonjwa ambao pia unafahamika kama PPR umewaathiri maelfu ya mbuzi huku 75,000 wakiwa tayari wakifariki. George Njogopa na taarifa kamili.

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)