Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wasomalia zaidi Waelezea Ugumu walio nao katika Kujitafutia Riziki

Wasomalia zaidi Waelezea Ugumu walio nao katika Kujitafutia Riziki

Kumeshuhudiwa kuongezeka kwa idadi wakimbizi wa ndani kwenye siku za hivi karibuni nchini Somalia ambao wanalalamikia ugumu wanaopitia katika kujitafutia riziki. Kwa muda wa majuma saba yaliyopita shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR limeandikisha wasomali 6000 ambao wamepitia magumu kama hayo hali inayosababishwa na ukosefu wa mvua na kutokuwepo usalama wa chakula. Wakimbizi 146 , 000 wamaendikishwa kuhama nchini Somalia mwaka huu. Pia kumekuwa na ripoti kuwa magari yanayosafarisha chakula na bidhaa zingine kutoka bandari ya Kismayo kwenda Afmadow na maeneo ya Lower Juba na Dobley yanakabiliana na vizuizi vya barabarani tangu juma lililopita. Adrian Edwards ni msemaji wa UNHCR.

CLIP