Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Waathirika wa Machafuko ya Sierra Leone Waanza Kulipwa Fidia

Waathirika wa Machafuko ya Sierra Leone Waanza Kulipwa Fidia

Kamishna ya kitaifa juu ya mpango wa kijamii imeanza kutoa fidia ya malipo ya fedha kwa waathirika zaidi ya 10,753 walioathiriwa na machafuko mabaya yaliyoikumba Sierra Leone miongo kadhaa iliyopita.

Machafuko hayo yaliyofikia ukomo mwaka 2000 yaligharimu maisha ya watu kadhaa huku wengine wakilazimika kukimbia uhamishoni kwa ajili ya kunusuru maisha yao.

Malipo hayo ambayo hugharimiwa kwa pamoja baina ya Umoja wa Mataifa kupitia fuko la ujenzi wa amani na kitengo kinachohusika na uhamiaji IOM, yanathamani ya dola za kimarekani 860,240 yatazambazwa nchi nzima katika kipindi cha majuma matatu.

Kwa wastani kila mwathirika anatazamiwa kupokea kiasi cha dola 80. Jumla ya waathirika waliotambulika hadi sasa wanafikia 32,148.