Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban Akaribisha Kukamilika kwa Mchakato wa Uchaguzi na Kutangazwa Rais Misri

Ban Akaribisha Kukamilika kwa Mchakato wa Uchaguzi na Kutangazwa Rais Misri

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amekaribisha hatua ya kukamilika kwa mchakato wa uchaguzi wa Rais nchini Misri kufuatiwa kutangazwa kwa matokeo rasmi ya uchaguzi wa duru ya pili uliyofanyika Juni 16 na 17 kutolewa na tume ya uchaguzi Jumapili.

Ban amewapongeza watu wa Misri kwa kuhakikisha mazingira ya amani na utulivu wakati wa uchaguzi huo.

Pia amempongeza Dr Mohamed Morsy kwa kuchaguliwa na kutangazwa kuwa Rais mpya wa Misri akisema anaamini Rais huyo hatopuuza matakwa ya watu wa Misri ya kuhakikisha kunakuwa na demokrasia, utekelezaji wa haki za binadamu, matumaini mapya na Misri isiyo na ghasia kwa manufaa ya watu wote wa taifa hilo la Afrika ya Kaskazini.