Annan ayataka mataifa yenye ushawishi mkubwa kushinikiza kukomeshwa kwa ghasia Syria

22 Juni 2012

Mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa nchi za Kiarabu, Kofi Annan, amesema aliunga mkono kikamilifu uamuzi wa Mkuu wa waangalizi wa Umoja wa Mataifa nchini Syria, UNSMIS, Jenerali Robert Mood kusitisha shughuli za UNSMIS nchini humo.

Annan ambaye ameandamana na mkuu wa UNSMIS, Meja Jenerali Robert Mood, amesema kwenye mkutano na waandishi wa habari kuwa waangalizi wa Umoja wa Mataifa walipelekwa Syria kuwasaidia watu wa Syria, na kwamba bado wanajitolea kufanya hivyo, lakini wanaweza tu kurejelea shughuli zao ikiwa hali ya usalama kuwaruhusu kufanya hivyo.

Ametoa wito kwa wahusika katika mzozo wa Syria kuitikia wito wa kimataifa, na kusitisha ghasia kwa njia zote zile, na kuyasihi mataifa yenye ushawishi mkubwa zaidi kuzishinikiza pande zote katika mgogoro huo kufanya hivyo.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter