Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano wa RIO+20 waingia siku ya mwisho

Mkutano wa RIO+20 waingia siku ya mwisho

Mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu maendeleo endelevu unakamilika leo mjini Rio-de Janeiro, Brazil, kwa hotuba kutoka kwa mataifa wanachama zaidi ya 50. Katika mahojiano na Radio ya Umoja wa Mataifa, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, ameelezea jinsi alivyofurahishwa na kutiwa moyo na kujitolea kwa viongozi wa kimataifa katika mkutano huo wa Rio. Amesifu kuunga kwao mkono mkataba thabiti uliofikiwa, na ambao amesema ni muhimu kwa ajili ya kuuwenga ulimwengi kwenye njia nzuri na endelevu.

Bwana Ban amesema atajadiliana na mataifa wanachama, jinsi ya kuweka kamati za wataalam wa kimataifa, ambao watashirikiana na tume ya viongozi muhimu, ili kukagua na kuwasilisha mitazamo ya baada kufikia malengo ya milenia mwaka 2015, na jinsi ya kuimarisha mpango wa mazingira wa Umoja wa Mataifa, na kuimarisha ufadhili. Amesema kuna mapendekezo mengine mengi muhimu ambayo yanahitaji kufuatiliwa kwa karibu, na ambayo yatajadiliwa kwenye mfumo mzima wa Umoja wa Mataifa.

(CLIP YA BAN)