Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban ataka mabadiliko nchini Misri kufanyika mapema

Ban ataka mabadiliko nchini Misri kufanyika mapema

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameonyesha kuunga mkono mabadiliko nchini Misri wakati taifa hilo linapoelekea kuwatimizia watu matarajio yao huku likijindaa kuingia kwenye uongozi wa kiraia.

Juma lililopita Misri iliandaa awamu ya pili ya uchaguzi wa urais ambao ndio kiungo muhimu cha mabadiliko kuelekea demokrasia, mabadiliko yaliyongo’a nanga mwezi Januari mwaka 2011.

Idara zinazosimamia uchaguzi nchini humo zinatarajiwa kutangaza matokeo rasmi ya uchaguzi huo siku ya Alhamisi kati ya Mohammed Mursi anayewakilisha chana cha Muslim Brotherhood na waziri mkuu wa zamani Ahmed Shafiq.