Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano wa Rio ni fursa ya kipekee na ya kihistoria:Ban

Mkutano wa Rio ni fursa ya kipekee na ya kihistoria:Ban

Mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu maendeleo endelevu umeanza rasmi katika mji mkuu wa Brazil, Rio de Janeiro. Kwa muda wa siku tatu zijazo, viongozi wa mataifa na serikali watawasilisha mitazamo yao kuhusu dunia endelevu ya siku zijazo katika mkutano huo wa Rio+20.

Huu ndio mkutano mkubwa zaidi katika historia ya Umoja wa Mataifa, na unatazamiwa kuwaleta pamoja watu 50, 000.

Akizungumza wakati wa kuufungua mkutano huo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, amesema mkutano wa Rio ni fursa ya kipekee, na labda ya mwisho ya kurekebisha mifumo ya maendeleo ya uharibifu na ufujaji wa rasilmali, na kuweka msingi wa maendeleo endelevu kwa ajili ya siku zijazo za mwanadamu.

(SAUTI YA BAN RIO)