Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hali Gaza bado ni tete- Ban

Hali Gaza bado ni tete- Ban

Hali katika eneo la Gaza bado ni tete, amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, ban Ki-Moon, katika ujumbe wake kwenye warsha ya waandishi wa habari kuhusu amani Mashariki ya Kati.

Bwana Ban amesisitiza wito wake wa kuruhusu kutembea na usafiri huru na salama kwa watu, vifaa vya ujenzi na bidhaa nyingine , na utekelezaji wa sehemu zote za azimio nambari 1860 la Baraza la Usalama.

Ameongeza kuwa ingawa Israel imejitahidi kwa kiasi fulani, juhudi zaidi zinahitajika, na kwamba Umoja wa Mataifa utaendelea kutekeleza wajibu wake katika kuzisaidia pande zote mbili kutafuta suluhu.