Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban ateuwa maafisa kadhaa

Ban ateuwa maafisa kadhaa

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amemteua Bi Amina J. Mohammed raia wa Nigeria kuwa mshauri wake katika masuala ya maendeleo na wakati huo huo ametangaza kumteua Parfait Onanga-Anyanga kutoka Gabon kuwa mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa nchini Burundi.

Bi Mohammed anatajwa kuwa na weledi wa hali ya juu hasa katika masuala ya maendeleo na amefanya kazi kwenye sekta hiyo kwa zaidi ya miaka 30.

Kadhalika mhadhali wa ngazi ya juu katika chuo kikuu cha Colombia na pia amepata kufanya kazi katika mradi wa malengo ya maendeleo ya mellenia.

Kuhusu uteuzi wa kuwa mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa nchini Burundi,Bwana Onanga anachukua nafasi inayoashwa na Bi Karina Landgren raia kutoka Sweden ambaye ameteuliwa kumwakilishi Katibu Mkuu nchini Liberia.