IOM Yazindua Kampeni ya Kulinda Watoto Dhidi ya Usafirishaji Haramu wa Watoto

1 Juni 2012

Shirika la Uhamiaji la Umoja wa Mataifa IOM, limezindua kampeni ya kuongeza ufahamu kuhusu siku ya kimataifa ya kulinda watoto, dhidi ya usafirishaji haramu wa watoto na kuwatumia katika kuombaomba.

Kampeni hiyo inayofadhiliwa na Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani, USAID, itawalenga mashabiki wa kandanda wanaozuru miji ya Ukraine ya Donetsk, Kharkiv, Kyiv na Lyiv kwa ajili ya mashindano ya EURO 2012 yanayoanza tarehe 8 Juni hadi Julai 1.

Kampeni hiyo ambayo inajumuisha taasisi za serikali zinazohusiana na maswala ya kuwalinda watoto katika miji hiyo minne na mashirika yasiyo ya kiserikali, ina lengo la kuondoa dhana kuwa kuwapa watoto wanao-ombaomba pesa kutayasaidia maisha yao, na kwamba kutawasaidia tu wale wanaowalazimu kuombaomba. Joshua Mmali na taarifa kamili.

(SAUTI YA JOSHUA MMALI)

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter