UM waitaka Tajikistan kuongeza fedha katika huduma ya Matatizo ya Akili

31 Mei 2012

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki ya afya Anand Grover ameitaka serikali ya Tajikistan kuongeza fedha za matumizi ya afya ili kufikia kiwango cha kimataifa na kuanzisha haraka mfuko wa fadhili wa huduma za afya utakaohakikisha fursa ya huduma za afya kwa wote.

Bwana Grover amekaribisha jkumu la serikali ya nchi hiyo la kuimarisha ufadhili wa sekta ya afya na kkumbatia mabadiliko. Amesema kuongeza matumizi ya afya kpewe kipaumbele ili kuhakikisha watu wote Tajikistan wana haki ya kupata hudma hiyo ikiwemo wenye matatizo ya afya ya akili. Akihitimisha ziara yake nchini humo amesema kwa ujumla mifumo ya sekta ya afya Tajikistan haijaendelea na haina ufadhili wa kutosha.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter