Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR Yabadili Makadirio ya Fedha zinazohitajika kama Msaada kwa eneo la Sahel

UNHCR Yabadili Makadirio ya Fedha zinazohitajika kama Msaada kwa eneo la Sahel

Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa, UNHCR, limebadilisha kwa kiasi kikubwa makadirio ya gharama ya msaada unaohitajika kuwasaidia mamia ya maelfu ya raia wa Mali walokimbia ghasia nchini mwao mapema mwaka huu.

UNCHR sasa linahitaji dola milioni 153.7 kwa ajili ya huduma zake mwaka huu kwenye mataifa ya Burkina Faso, Mali, Mauritania na Niger. Mahitaji haya yamepanda kwa kiasi kikubwa tokea dola milioni 35.6 mwezi Februari mwaka huu.

Kufuatia mapigano ya wanamgambo wenye asili ya Tuareg mnamo mwezi Januari na mzozo ulokithiri baada mapinduzi ya mwezi Machi na ongezeko la makundi yenye silaha kaskazini mwa Mali, takriban watu 320, 000 raia wa Mali wamekimbilia nchi jirani za Burkina Faso, Mauritania na Niger au kwenye maeneo salama ndani mwa Mali. Flora Nducha na taarifa kamili

(TAARIFA YA FLORA NDUCHA)