Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mauaji ya El Houleh huenda yakachukuliwa kuwa uhalifu dhidi ya ubinadamu:Pillay

Mauaji ya El Houleh huenda yakachukuliwa kuwa uhalifu dhidi ya ubinadamu:Pillay

Kamishina mkuu wa haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa Navi Pillay amesema kuwa visa vya mauaji ya wanavijiji katika eneo la El Houleh mjini Homs nchini Syria huenda vikaorodheshwa kuwa uhalifu dhidi ya ubinadamu . Kulingana na uchunguzi wa Umoja wa Mataifa watu 108 waliuawa 49 kati yao wakiwa ni watoto huku 39 wakiwa ni wanawake.

Msemaji wa Pillay, Rupert Colville amesema kuwa uchunguzi wa Umoja wa Mataifa unaonyesha kuwa karibu watu 20 waliuawa kupitia mashambulizi ya mabomu mabomu akiongeza kuwa kuwa wengi wa waliouwa walikuwa makwao.

(SAUTI YA RUPERT COLVILLE)

Uchunguzi uliofanywa ulilinyooshea kidole cha lawama kundi la Shabiha lililo na uhusiano wa karibu na jeshi la Syria. Ofisi ya haki za binadamu inalitaka baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kubuni tume ambayo itaruhusiwa kuingia nchini Syria kufanya uchunguzi