Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Pillay ahimiza Zimbabwe kufanya Uchaguzi Huru na wa Haki

Pillay ahimiza Zimbabwe kufanya Uchaguzi Huru na wa Haki

Kamishina mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Navi Pillay anahitimisha ziara yake nchini Zimbabwe alikokwenda kutathimini hali ya haki za binadamu.

Bi Pillay ambaye akiwa nchini humo amekutana na Rais wa nchi hiyo, waziri mkuu, wanaharakati wa haki za binadamu na jumuiya za kijamii, amempongeza Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe kwa kutoa wito wa kwamba katika uchaguzi mkuu ujao hakutakuwa na ghasia, na Pillay amemtaka Rais Mugabe kutimiza kauli hiyo.

Pillay amemtaka Rais Mugabe kuhakikisha kwamba uchaguzi huo ujao utakuwa huru, wa haki na usio ambatana na ghasia, pia uchaguzi utakaojumuisha wote na kuzingatia matakwa ya watu wa Zimbabwe.

(SAUTI YA NAVI PILLAY)

Naye waziri Mkuu wa nchi hiyo Morgan Tsvangirai amesema tangu kuanzishwa kwa serikali ya Umoja wa kitaifa kuna hata ambazo zimepigwa nchini Zimbabwe.

(SAUTI YA NAVI PILLAY)