Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ILO yaonya kuhusu kutoweka kwa uhusiano kati ya Siasa na Watu

ILO yaonya kuhusu kutoweka kwa uhusiano kati ya Siasa na Watu

Mkuu wa Shirika la Wafanyakazi duniani, Juan Somavia, ameonya kuwa uhusiano kati ya watu wa kawaida na serikali au sera za kisiasa, unaendelea kudidimia.

Somavia ameyasema haya wakati akiwahutubia vijana wanaohudhuria kongamano la ajira kwa vijana mjini Geneva.

Amesema kuwa watu wengi, hasa vijana, wanaendelea kujitenga na serikali na sera za kisiasa kwa sababu wanahisi kama serikali haziwatilii maanani au kuwahusisha katika mstakabala mzima wa kutayarisha au kuziamulia hizo sera.

Zaidi ya asilimia 70 ya watu wasokuwa na ajira Afrika ya Kusini ni vijana, kwa mujibu wa Mratibu wa Maswala ya Vijana katika chama cha wafanyakazi Afrika ya Kusini, Phindile Kunene, ambaye ni mmoja wa vijana mia 100 wanaokutana mjini Geneva

(SAUTI YA PHINDILE KUNENE)

Mkuu wa ILO Ameonya pia kuhusu watu kutoridhika na jinsi mdororo wa kiuchumi ulivyoshughulikiwa katika bara la Ulaya, huku akiyasifu mataifa yanayoendelea kwa kufuata mkondo tofauti ulowakinga watu kutokana na athari za mdororo wa uchumi duniani.