Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Amos aunga mkono jitihada za Burkina Faso za kukabiliana na Tatizo la Uhaba wa Chakula

Amos aunga mkono jitihada za Burkina Faso za kukabiliana na Tatizo la Uhaba wa Chakula

Mkuu wa masuala ya kibinadamu kwenye Umoja wa Mataifa Valerie Amos amesema kuwa Umoja wa Mataifa na washirika wake wanafanya jitihada za kulisaidia taifa la Burkina Faso kukabiliana na tatizo la uhaba wa chakula ambalo limewaathiri karibu watu milioni 2.8 wakiwemo wakimbizi 60,000 kutoka Mali.

Amos amekamilisha ziara yake nchini Burkina Faso ambapo aliutembeea mji mkuu Ouagadougou pamoja na miji ya Djibo, Mentao na Ingani iliyo kaskazini. Amos alikutana na rais wa nchi hiyo pamoja na waziri ambapo walijadili mipango ya serikali na kukagua huduma za mashirika ya kibinadamu nchini Humo. Alice Kariuki na taarifa kamili.

(SAUTI YA ALICE KARIUKI)