Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mwendesha mashitaka wa ICC ashinikiza kukamatwa kwa waasi wanaofanya uhalifu DR Congo

Mwendesha mashitaka wa ICC ashinikiza kukamatwa kwa waasi wanaofanya uhalifu DR Congo

Mwendesha mashitaka mkuu wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC anatafuta makosa mapya ya uhalifu wa vita dhidi ya kiongozi wa waasi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Bosco Ntaganda.

Luis Moreno-Ocampo anamshutumu bwana Ntaganda kwa mauaji,mauji ya kikabila, ubakaji na utumwa wa ngono. Mwendesha mashitaka huyo wa ICC pia anatafuta makosa kama hayo dhidi ya Sylvestre Mudacumura, kamanda wa vikosi vya kundi la waasi kutoka Rwanda la FDLR.

Bwana Moreno-Ocampo amesema ametoa tangazo kwa umma akiwa kwa Umoja wa mataifa ili kufikisha ujumbe huu maalumu.

(SAUTI YA OCAMPO)

“Wafuasi wa Ntaganda na Mudacumura lazima waelewe kwamba ni wakati wao wa kujiengua na kuacha uhalifu, na hara kusaidia kukamatwa wa viongozi hao.”

Pia Ocampo amesema mipango ya serikali kushambulia makundi haya lazima itilie manaani ukweli kwamba operesheni za kijeshi za nyuma dhidi ya waasi hawa zilisababisha mauaji kwa raia hivyo ni wakati wa kuikarabati mipango hiyo na kutumai kwamba jeshi la Congo na la Rwanda kama litahusika yatabadilisha operesheni hizi za kijeshi na ziwe za kuwakamata.