Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakimbizi wa DRC walio Congo kurudi nyumbani

Wakimbizi wa DRC walio Congo kurudi nyumbani

Zaidi ya wakimbizi 81,000 kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo watarejeshwa makwao kutoka taifa jirani la Congo ambapo wamekuwa wakiishi kwa muda wa miaka mitatu iliyopita kwenye shughuli iliyopangwa na shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR.

Wakimbizi hao walikimbia mapigano ya kikabila katika mkoa ulio kaskazini mwa DRC wa Equator mwaka 2009. Zaidi ya watu 143,000 walilazimika kuhama makwao kutokana na ghasia za kikabila kufuatia kuwepo kwa tofauti za uvuvi na ukulima. Andrej Mahecic ni kutoka UNHCR.

SAUTI YA ANDREJ MAHECIC