Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Yemen kwenye hatari ya kukumbwa na janga la kibinadamu

Yemen kwenye hatari ya kukumbwa na janga la kibinadamu

Mashirika ya Umoja wa Mataifa yanasema kuwa huenda Yemen ikakumbwa na janga la kibinadamu iwapo ufadhili wa dharura hautatolewa kushughulikia tatizo la utapiamlo na magonjwa.

Hali iliyopo kwa sasa imechochewa na ukosefu wa usalama ambapo watu wamebaki bila chakula wakati ambapo uharibifu kwenye vituo vya afya na ukosefu wa madawa vikichangia maambukizi ya magonjwa kama Surua na Polio.

Shirika la kuwahudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF linasema kuwa karibu watoto 270,000 huenda wakafa miezi inayokuja kutokana na utapiamlo likiongeza kuwa asilimia 60 ya watoto nchini Yemen wana matatizo ya kukua. Marixie Mercado ni kutoka UNICEF.

SAUTI YA MARIXIE MERCADO