Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wananchi wa Syria wana matumaini makubwa kwa UNSMIS:MOOD

Wananchi wa Syria wana matumaini makubwa kwa UNSMIS:MOOD

Mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Syria UNSMIS Meja Jenerali Robert Mood amesema kuwa wananchi wa Syria wameweka matumaini yao kwenye ujumbe huo. Akiongea na Radio ya Umoja wa Mataifa hii leo Meja Mood amesema kuwa mashambulizi mabaya ya mabomu yaliyofanyika nchini Syria ni kumbusho la matatizo wanayopitia wananchi wa Syria.

SAUTI YA ROBERT MOOD

Meja Mood anasema kuwa hadi sasa waangalizi kutoka nchi 27wako kwenye miji sita nchini Syria na huenda idadi yao ikafikia waangalizi 300 majuma yanayokuja.