Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban ataka nchi za kiarabu kusaidiwa ili ziweze kuwa na demokrasia

Ban ataka nchi za kiarabu kusaidiwa ili ziweze kuwa na demokrasia

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki- moon ameushauri ulimwengu kuunga mkono jitihada za wenyeji wa mashariki ya kati za kuwa na demokrasia haki za masusla ya kijamii. Kupitia ujumbe wake wakati wa ufunguzi wa mkutano wa siku mbili wa mawaziri wa tume wa uchumi ya Umoja wa Mataifa eneo la Sahara Magharibi ulioanza leo mjini Beirut nchini Lebanon Ban amesema kuwa watu wa mshariki ya kati wameonyesha ishara ya kuleta mabadiliko.

Kwenye ujumbe uliosomwa kwa niaba yake na mjumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Lebanon Derek Plumbly Ban amemema kuwa changamoto kwa sasa ni kupatikana suluhu la shinikizo la wanachi wakati wanapoamua kutisha haki na uhuru wao.