Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban akaribisha Urusi na Marekani kusaini mkataba wa nyuklia

Ban akaribisha Urusi na Marekani kusaini mkataba wa nyuklia

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon amekaribisha kura ya bunge la Marekani ya kuunga mkono kuidhinishwa kwa mkataba wa kupunguza zana za nyuklia uliotiwa sahihi mapema mwaka huu kati ya viongoiz wa Urusi na Marekani.

Rais wa Mareknai Barack Obama pamoja na rais Dmitry Medvedev wa Urusi walitia sahihi makataba huo mwezi Aprili mwaka huu na kuahidi kupunguza zana zao za kinyuklia. Kwenye ujumbe kupitia kwa msemaji wake, Ban amesema kuwa hatua ya marekani ni mwanzo mpya wa mkataba wa kupunguza zana za nyuklia.

Ban amesema kuwa anaamini nchi hizo mbili zitakuwa na ushirikiano na kuendelewa kufuatilia suala hilo kuhakikisha kuwa zimepunguza zana hizo. Ban ameongeza kuwa amejitolea kuhakikisha kuwa mkataba huo umetekelezwa.