Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban ataka viongozi wa dunia kupigania matunda ya pamoja

Ban ataka viongozi wa dunia kupigania matunda ya pamoja

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amewataka viongozi wa dunia kujitolea na kuanza kuyapa uzito wa pekee masuala yatayozaa matunda mema kwa binadamu wote.

Amesema ni muhumu sana kushuhudia viongozi wa dunia wakiweka dhamira ya dhati kuwaletea wananchi wao usawa na haki, hasa katika wakati huu ambako kunashuhudia kuongezeka kwa matukio yanayofinya na kunyima haki, ukosefu wa usalama.

Ban ambaye alikuwa akizungumza kwenye dhifa ya utowaji zawadi katika baraza la Atlantic amesema kuwa kufanya hivyo ni kutimiza matakwa ya uanzishwaji wa Umoja wa Mataifa.

Amesema kuna umuhimu sasa kwa viongozi wa dunia kuwa na utashi utakahakikisha dunia inasalia kuwa na matunda mema kwa wote.