Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

CITES yaipongeza Uchina kwa sheria ya kulinda wanyama pori

CITES yaipongeza Uchina kwa sheria ya kulinda wanyama pori

Mkataba wa kimataifa wa biashara ya vuimbe vilivyo katika hatari ya kutoweka  CITES umeitunikia Uchina chetio cha pongezi kupitia shirika lake la kitaifa NICECG kwa kutambua sheria zake mbili za operesheni za kulinda wanyama pori zilizopitishwa mapema mwaka huu.

Zaidi ya maafisa wa polisi 100,000 wameandaliwa kuendesha operesheni ya kupambana na uhalifu dhidi ya wanyama pori.

Katika operesheni hiyo iliyoandaliwa na uongozi wa kitaifa wa hifadhi ya misitu, zaidi ya visa 700 vya biashara haramu ya wanyama pori vilibainika, maduka 7,155 haramu ya vitu vya wanyama pori na maduka mengine 628 ya kwenye mtandao yanayoza vifaa vya wanyama pori yamefungwa.

Kwa mujibu wa CITES tovuti 520 zinazoaminika kufanya biashara haramu ya wanyama pori zinafuatiliwa kwa karibu ikiwa ni miongoni mwa hatua zinazochukuliwa na serikali ya Uchina.