Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WFP kusafirisha misaada ya chakula kwenda Comoro

WFP kusafirisha misaada ya chakula kwenda Comoro

 

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP linatarajiwa kuongoza shughuli ya usafirishaji wa tani 28 za biskuti vya hali ya juu kwa njia ya ndege kwenda nchini Comoro nchi iliyokumbwa na mafuriko na maporoko ya udongo.

Kulingana na ukaguzi uliofanywa na shirika la WFP unaonyesha kuwa watu 12 kwenye visiwa vyote vitatu vya Comoro wanahitaji misaada ya dharura ya chakula. Shughuli hiyo inatarajiwa kung’oa nanga siku ya Jumatano ambapo usafirishaji wa misaada baada ya kuwasili kwenda visiwa vya Anjuan na Moreli ukitarajiwa kufanywa kwa njia ya mashua.

Takriban watu 57,232 wanahitaji misaada ya dharura huku nyumba 2000 zikiharibiwa na kuacha karibu familia 4000 bila makao.