Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNAIDS yazindua kampeni kumaliza maambukizi ya HIV kwa watoto

UNAIDS yazindua kampeni kumaliza maambukizi ya HIV kwa watoto

Shirika la kupambana na ugonjwa wa Ukimwi la Umoja wa Mataifa UNAIDS lina mipango ya kumaliza maambukizi ya virusi vya ukimwi miongoni mwa watoto ifikapo mwaka 2015. Kupitia kwa kampnei yake yenye kichwa “Iamini. Ifanye.”

UNAIDS pia inalenga kuhakikisha kuwa wanawake wanaoishi na virusi vya ukimwi wanakuwa na afya wakiwa waja wazito, wanapojifungua na wanaponyonyesha.

UNAIDS inakadiria kwamba karibu watoto 390,000 wanaambukizwa virusi vya ukimwi kila mwaka huku wanawake 42,000 wakifa kutokana na matatizo ya HIV na uja uzito. Sakuya Oka ni msemaji wa UNAIDS.

(SAUTI YA SAKUYA OKA)