Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakimbizi wa kisomali wawasili kwenye pwani ya Malta

Wakimbizi wa kisomali wawasili kwenye pwani ya Malta

Waanga wenye uchovu waliokuwa kwenye mashua iliyokuwa ikiwasafirisha wakimbizi kutoka Somalia iliyowasili kwenye pawani ya Malta wameliambia shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR kwamba wanaume watano na wanawake wawili waliokuwa kwenye mashua hiyo waliaga dunia kwenye safari hiyo ndefu iliyoanzia nchini Libya.

Hii ndiyo mashua ya pili kuwasili kwenye pwani ya Malta mwaka huu na kufikisha idadi yote ya watu kuwa 210. Idadi ya watu waliokufa wakijaribu kuingia kwa mashua barani Ulaya mwaka huu imetimu watu 81. Adrian Edwards ni msemaji wa UNHCR.

(SAUTI YA ADRIAN EDWARDS)