Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM yasambaza misaada kwa wakimbizi kutoka Syria walio kaskazini mwa Iraq

IOM yasambaza misaada kwa wakimbizi kutoka Syria walio kaskazini mwa Iraq

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM kwa ushirikiano na shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa wamesambaza misaada ya dharura isiyokuwa chakula kwa familia 98 kutoka Syria zilizowasili kwenye kambi ya Domiz kwenye eneo la Dahuk kaskazini mwa Iraq.

Misaada hiyo inajumuisha mablanketi, vyombo vya maji, mitungi ya gesi, matandiko, taa na nyinginezo iliyotolewa na IOM pamoja na mito ya kulalia, taa zinazotumia mafuta na vifaa vingine vya usafi kutoka kwa shirika la UNHCR. IOM imetoa misaada kama hiyo kwa wakimbizi 1551 kutoka Syria kwenye kambi ya Domiz kufuatia ombi kutoka kwa usimamizi wa eneo la Dahuk. Jumbe Omari Jumbe ni afisa wa IOM.

(SAUTI YA JUMBE OMARI JUMBE)