Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkuu wa UNMISS azitaka jamii kuanza ukurasa mpya wa amani

Mkuu wa UNMISS azitaka jamii kuanza ukurasa mpya wa amani

 

Mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu nchini Sudan Kusini ambaye pia ni mkuu wa mpango wa kulinda amani nchini humo UNMISS Hilde Johnson amezitaka jamii za Jonglei kuanza ukurasa mpya wa amani. Akizungumza katika hafla ya ufungaji mkutano wa amani wa jamii za Jonglei mjini Bor Jonglei amesema leo ni fursa nzuri kwa wat wa jamii hizo kusema visa sasa basi.

Wawakilishi kutoka jamii kubwa sita zikiwemo Dinka, Kachipo, Jie, Nuer, Anyuak na Murle wamehudhuria mktano huo na kutia saini maazimio mhimu ya kumaliza mzunguko wa machafuko na kutekeleza mpango wa amani wa Jonglei.

Bi Johnson amesema wanataka kuona amani kuanzia mashinani, kwenye makambi ya ng’ombe na kwenye jamii zote.

Amesisitiza kwa amani ya kdumu itapatikana tuu endapo suluhu ya changamoto za Jonglei itapatikana, wakati ambapo taasisi za usalama zitaanzishwa na ulinzi kwa watu utakuwepo. Mchungaji John Okumu ni msemaji wa kamati ya amani ya Rais.

(SAUTI YA JOHN OKUMU)