Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Msaada wa chakula Sahel inamaanisha kuokoa maisha kwa mamia

Msaada wa chakula Sahel inamaanisha kuokoa maisha kwa mamia

Msaada wa chakula kwa mamilioni ya watoto kwenye eneo la Sahel Afrika ya Magharibi inamaanisha tofauti ya maisha na kifo kwa watoto wa eneo hilo amesema mkuu wa shirika la mpango wa chakula duniani WFP Bi Ertharin Cousin.

Bi Cousin ambaye yuko ziarani kwenye jimbo hilo amesma kwamba dola zaidi ya milioni 400 zinahitajika haraka ili kugawa msaada wa chakula kwa watu zaidi ya milioni 8 walioathirika na ukame Sahel.

Ameongeza kuwa Jumapili alitembelea jamii ambayo haijapata msaada wa chakula na kujionea athari za utapia mlo kwa watoto.

(SAUTI YA ERTHARIN COUSIN)