Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tishio la ugaidi bado lipo duniani:Ban

Tishio la ugaidi bado lipo duniani:Ban

Serikali kote duniani wanahitaji kuendelea kufanya kazi pamoja kupunguza hatari ya ugaidi amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon siku ya Ijumaa.

Bwana Ban, akizungumza kwenye mkutano kuhusu ugaidi kwenye Baraza la Usalama amependekeza kuimarisha masuala ya sheria na kukabiliana na watu wanaochagiza itikadi kali. Amesema jumuiya ya kimataifa inaendelea kufuatilia na kuchukua hatua kukabiliana na ugaidi duniani.

(SAUTI YA BAN KI-MOON)

Juhudi za pamoja zimesaidia kuingilia mashambulizi na kuvuruga mitandao ya kigaidi, lakini mashambulizi ya karibuni Afghanistan, Iraq, Nigeria na Yemen yanadhihirisha kwamba tishio la ugaidi bado lipo.

Makundi ya kigaidi yanaendelea kutafuta mahali pa kujihifadhi, yanatumia mbinu mpya na kutafuta mahali pa kushambulia. Ban anapendekeza kuanzishwa kwa cheo cha mratibu wa Umoja wa Mataifa wa masuala ya ugaidi.