Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watoto milioni moja kwenye hatari ya kufa njaa Sahel:UNICEF

Watoto milioni moja kwenye hatari ya kufa njaa Sahel:UNICEF

Shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF linasema kuwa takriban watoto milioni moja wako kenye hatari ya kufa kutokana na tatizo la utapiamlo kwenye eneo la sahel lililo katikati na magharibi mwa bara la Afrika hali ambayo imechangiwa na ukame. Mkurugenzi wa huduma za UNICEF Louis Georges Arsenault amesema kuwa kulingana na makadirio ya mwaka 2012 kuna zaidi ya watoto milioni moja wanaosumbuliwa na utapiamlo akiongeza kuwa kunahitajika kuchukuliwa hatua za mapema kabla haijakuwa vigumu kuyaokoa maisha.

Kwa sasa kuna takriban watu milioni 15 wanaokabiliwa na utapiamlo kwenye eneo la Sahel kutoka habari ya Atlantic hadi bahari ya Shamu. Nchi ambazo watu wanakabiliwa na uhaba wa chakula ni pamoja na Burkina Faso, Chad, Mali, Mauritania, Niger na sehemu za kaskazini mwa Cameroon, Nigeria na Senegal.