Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM yatoa huduma za maji na usafi kwa wakimbzi kwenye jimbo la Abyei

IOM yatoa huduma za maji na usafi kwa wakimbzi kwenye jimbo la Abyei

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM limeanza kutoa huduma za maji na vifaa vingine vya usafi kwa watu 700 kwenye eneo la Abyei waliolazimika kuhama makwao kufuatia makabiliano ya kijeshi kati ya Sudan na Sudan kusini. Familia hizo zinazojumuisha idadi kubwa ya wanawake na watoto walihama makwao tarehe 21 Aprili 2012 kutoka kijiji cha Abiemnom kwenye jimbo la Unity lililo Sudan Kusini wakati kulipoanza mapigano.

Usambazaji wa misaada ikiwemo mitungi ya maji na dawa na kutibu maji ulianza tarehe 23 mwezi huu huku IOM ikiwahamisha waliohama makwao kuhusu usafi. Jumbe Omari Jumbe ni msemaji wa IOM.

(SAUTI YA JUMBE OMAR JUMBE)