Mashirika ya UM yataka kutolewa misaada kuwasaidia waathiriwa wa mafuriko Pakistan

26 Aprili 2012

Maafisa wa ngazi za juu kuhusu masuala ya kibinadamu kwenye Umoja wa Mataifa wamepongeza jitihada zinazoendelea za kuwasaidia watu milioni 7.2 walioathiriwa na mafuriko nchini Pakistan. Mkurugenzi wa huduma za shirika la kuratibu masuala ya kibinadamu la Umoja wa Mataifa OCHA John Ging amesema ameona huduma zinazotolewa na mashirika ya kutoa misaada na serikali ya Pakistna alipofanya ziara ya siku tatu nchini humo.

Serikali ya Pakistan na mashirika ya kutoa misaada ya kibindamu wamekuwa wakishirikiana kwenye mikoa ya Sindh na Balochistan kuwasaiadia watu milioni 5.2 walioathiriwa na mafuriko ya mwaka uliopita.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter