Coomaraswamy aelezea dhuluma kwenye mpaka kati ya Sudan na Sudan Kusini

25 Aprili 2012

Mjumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu watoto na mizozo Radhika Coomaraswamy ameelezea hofu yake kufuatia makabiliano ya hivi majuzi kwenye sehemu zinazopakana na Sudan na Sudan Kusini huku athari zaidi ikiwaangukia watoto. K

Kuliripotiwa vifo vya watoto wawili wa kiume wakati kulipoendeshwa mashambulizi ya anga kwenye soko la Rubkona jimbo la Unity. Coomaraswamy amesema kuwa mashambulizi kwenye maeneo yaliyo na idadi kubwa ya watu ni ukiukaji wa sheria ya kimataifa.

Makabiliano kati ya mataifa hayo mawili yamechacha majuma machache yaliyopita baada ya Sudan kulinyakua eneo lenye utajiri wa mafuta la Heglig lililo kwenye jimbo la Kordofan Kusini.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter