Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maelfu wakimbia mapigano kati ya Sudan na Sudan Kusini

Maelfu wakimbia mapigano kati ya Sudan na Sudan Kusini

Shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR linasema kuwa karibu watu 35,000 wamelazimika kuhama makwao kufuatia mapigano kati ya Sudan na Sudan Kusini. Waliohama wanatoka kwenye maeneo yanayolizunguka maeneo yenye utajiri wa mafuta linalozozaniwa la Heglig, Talodi na sehemu za Kordofan Kusini.

UNHCR inaelezea wasi wasi wake kuhusiana na hatma ya karibu wakimbizi 20,000 walio kwenye kambi karibu na mpaka ambapo limewashauri kuhamia maeneo salama. Adrian Edwards kutoka UNHCR anasema kuwa wakimbizi 2000 tayari wamehamishwa.

(SAUTI YA ADRIAN EDWARDS)