Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban akaribisha uamuzi wa Baraza la Usalama kuanzisha UNSMIS

Ban akaribisha uamuzi wa Baraza la Usalama kuanzisha UNSMIS

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amekaribisha uamuzi wa pamoja uliopitishwa na baraza la usalama la Umoja wa Mataifa Jumamosi April 21 wa kuidhinisha mpango wa Umoja wa Mataifa wa uangalizi Syria UNSMIS ambao mwanzo utakuwa ni wa siku 90.

Ban ameitaka serikali ya Syria na pande zote kuweka mazingira ambayo ni muhimu na ya lazima kwa kupelkwa mpango huo na amesisitiza haja ya serikali kumaliza ghasia na ukiukwaji wa haki za binadamu hususan kusitisha matumizi ya silaha nzito dhidi ya raia, kuondoa silaha hizo na wanajeshi kwenye maeneo ya raia.

Ban amesema anatarajia serikali ya Syria kuhakikisha utendaji wa UNSMIS ikiwa ni pamoja nakuwapa fursa na uhuru wakutembea na kufikia maeneo mbalimbali,kutoingilia mawasiliano yao na kuwahakikishia usalama.

Katibu Mkuu ameongeza kuwa anatrajia utekelezaji wa makubaliano baina ya Umoja wa Mataifa na serikali ya Syria kuhusu usafirishaji wa anga kama ilivyoainishwa na Baraza la Usalama. Amezitaka pande zote hasimu nchini Syria kutoa ushirikiano kwa mpango wa UNSMIS.